Thursday, October 30, 2014

MHE.NAGU ASHUHUDIUA UWEKAJI WA SAINI MAKUBALIANO YA FURNITURE CENTER NA TAWOFE


MHE.NAGU ASHUHUDIUA UWEKAJI WA SAINI MAKUBALIANO YA FURNITURE CENTER NA TAWOFE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu akiangalia samani wakati wa sherehe fupi ya uwekaji  saini makubaliano kati ya Funiture Center DSM na Shirikisho la Mafundi Samani Tanzania (TAWOFE) katika ofisi za Furniture Center Dar es Salaam.
  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu akishudui uwekaji saini makubaliano kati ya Funiture Center DSM na Shirikisho la Mafundi Samani Tanzania (TAWOFE) tarehe 29 Oktoba, 2014 katika ofisi za Furniture Center Dar es Salaam. Makubaliano hayo, ni kuimarisha ushirikiano kwa kuingia ubia na wazalishaji wakubwa kama Furniture Center ili kunufaika na uwezo wao mkubwa kwenye maeneo muhimu kama mitaji, masoko ya bidhaa, teknolojia na vifaa vya kisasa vinavyofaa kutengenezea samani hizo.
Mhe. Nangu alisema, "ushirikiano wa namna hii utaboresha ununuzi wa bidhaa zinazopatikana nchini kwa urahisi na kukuza soko letu pia huu ni uzalendo wa hali ya juu uliooneshwa katika kuwawezesha mafundi samani kuingia katika soko la Kimataifa, wakijiamini kwamba bidhaa zao zina ubora wa Kimataifa na kupongeza uongozi wa Funiture Center DSM kwa hatua walioichukua".