Pichani (wa tatu kulia),Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor Kikoti akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo katika ofisi zao zilizopo jengo la Millenium Tower,Kijitonyama jijini Dar,kuhusiana na kufanyika kwa mkutano wao wa 7 wa mwaka wa wadau kuanzia Oktoba 23 mpaka 24, 2014.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano (AICC),jijini Arusha.Bwa.Victor amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni '' kusherehekea miaka 70 ya ukuaji na huduma bora kwa Wanachama''. '' Kauli mbiu hii imefikiwa baada ya mfuko kutimiza miaka 70 tangu ulipoanzishwa mwaka 1944,ambapo Wadau wa mkutano huo watajadili kwa kina juu ya huduma za LAPF kwa miaka 70iliyopita pamoja na kushiriki mafanikio ya mfuko kwa pamoja.
Matekelezo Mfuko wa Pensheniwa LAPF,Bwa.Victor Kikoti amesema kuwa,Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwaWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.Hawa Ghasia
Pichani kulia ni Meneja Mkoa Bwa.Ramadhani Mkeyange,Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata pamoja na Meneja wa Kanda ya Dar,Bi.Amina Kassim
Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata,akifafanua moja ya swali aliloulizwa na Waandishi wa Habari kuwa mfuko wa LAPF unaendelea kujivunia mafanikio ya kuwa mfuko unaokuwa kwa kasi hapa nchini pamoja na kuwa bora kwa miaka mitano mfululi kwenye suala zima la uwajibikaji na utunzaji wa vitabu.
Amesema kuwa mfuko pia utazindua logo mpya inayotumika,ambayo inaashiria ukuaji wa mfuko huo na dhamira yao ya kuendelea kukua zaidi na kuboresha huduma kwa wanachama wao,ameongeza kusema kuwa mfuko huo utatoa fursa mpya ya mkopo wa elimu kwa wanachama wake ilivyozinduliwa mwezi Agosti mwaka huu.
Pichani ni baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa LAPF.