Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kushoto) akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekeleza wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa (wa pili kulia) mara baada ya kuhudhuria hivi karibuni maabara inayochambua miradi ya afya itakayoingia katika BRN. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt, Mohammed Saleh Jidawi (kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa), Hawa Ghasia akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud Thabit Kombo wakati viongozi hao walipotembelea maabara inayochambua miradi ya afya itakayoingia katika BRN.
Baadhi ya wawakilishi wa Wabia wa Maendeleo waliopo nchini wakifuatilia majadiliano jana jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea maabara ambayo inachambua miradi ya sekta ya afya itakayoingizwa katika BRN.
Badhi ya washiriki wa maabara inayojadili miradi ya afya itakayoingizwa katika BRN wakifurahia zawadi waliyopewa na Waziri wa Afya (hayuko pichani) baada ya kundi lao kushinda katika uwasilishaji wa miradi ya afya itakayochambuliwa zaidi ili kuingia katika BRN.