Thursday, October 09, 2014

MAKAMU WA RAIS WA TIMU YA JAMHURI YA PEMBA BW.SULEIMAN SALEH AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA SHILINGI MILIONI 8 MJINI WETE PEMBA



MAKAMU WA RAIS WA TIMU YA JAMHURI YA PEMBA BW.SULEIMAN SALEH AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA SHILINGI MILIONI 8 MJINI WETE PEMBA Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.
Bw.Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo viatu, mipira, nyavu za magoli na vifaa mbali mbali vya mazoezi ili kuihamasisha timu hiyo ambayo mwaka 2003 walikuwa mabingwa Zanzibar na miaka ya 2008 na 2011 ilishiriki katika klabu bingwa Afrika ambapo ilitolewa na St.George ya Ethiopia na Hangwe FC ya Zimbabwe.
Bw. Suleiman Saleh ambaye akikabidhi msaada huo mjini Wete, Pemba,  jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba. 
Katika kujiwekea malengo ya kucheza tena kimataifa katika miaka mitatu ijayo Jamhuri inayoundwa na vijana wadogo imeandaa mkakati maalum kukamilisha azma yao hiyo.