Na Editha Karlo wa
Globu ya jamii Kigoma
Mpaka sasa jumla ya maiti nne zimeopolewa na kufanya kufikia idadi ya maiti kumi zimepatikana katika ajali ya mitumbwi iliyotokea jana mchana katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi iliyokuwa imebeba maharusi ndugu jamaa na wapambe kupigwa wimbi na kuzama.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya Mkoa amesema kuwa bado idadi maiti zilipo kwenye maji ni kubwa ambazo bado hazijapatikana.
''Zoezi hili linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu duni ambavyo ni kikwazo katika zoezi hili la ukoaji. Lakini bado tunaendelea na kazi ''Mkuu wa Mkoa huyo ameiambia Globu ya Jamii asubuhi hii.
Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana. Nao ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya (wa pili kushoto) anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Kigoma
Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana katika ziwa Tanganyika baada ya ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo
Wanajeshi wa Jeshi la Wananch (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama
Zoezi la uopoaji wa miili linaendelea na vikosi mbalimbali vya ukoaji katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana