Friday, October 31, 2014

Kongamano la Ufugaji nyuki Barani Afrika kufanyika Jijini Arusha



Kongamano la Ufugaji nyuki Barani Afrika kufanyika Jijini Arusha
 Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (Kitengo cha Misitu na Nyuki),Bi. Gladnes Mkamba akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu uwepo wa Kongamano la Ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Novemba 11 - 16,2014 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC),jijini Arusha.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu kutoka Wakala wa Misitu Tanzania,Bw. Zawadi Mbwambo.Picha na Othman Michuzi.
Kaimu Mkurugenzi Mwandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (Kitengo cha Ufugaji Nyuki),Bi. Monica Kagya akichangia machache kuhusu Kongamano hilo na umuhimu wa wadau kushiriki.