Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwa katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kalenga, Iringa Vijini, walipoanza ziara ya siku sita za kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za watu na kuzitafutia ufumbuzi.Katika mkutano huo Kinana aliitaka Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwatafutia soko la uhakika wakulima.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akivishwa vazi la kimila la wazee wa kabila la Wahehe ikiwa ni heshima kwake.
Kinana akivishwa kilemba
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila baada ya kukabidhiwa mkuki.
Kinana akiwa amekaa na Chifu Abdul Mkwawa pamoja na wazee wa kimila wa kabila la wahehe.
Kinana akipendeza na vazi la kihehe huku akiwa na mkuki mkononi.
Kinana akihutubia katika mkutano huo huku akiwa amevalia kimila.
Kinana akihutubia huku akiwa juu ya kichuguu alichokuwa akikitumia Chifu Mkwawa enzi hizo kuwahutubia wananchi wake.
Kinana akishiriki kuvua samaki katika moja ya mabwawa ya umoja wa akina mama Kata ya Kalenga.
Kinana akishiriki kupulizia dawa katika shamba la mfano la nyanya katika Kata ya Kalenga.
Kinana akiongozana na wananchi baada ya kukagua mradi wa ufugaji samaki na shamba la nyanya katika Kata ya Kalenga
Kinana akiwa na Balozi wa Shina la CCM namba moja Kata ya Kalenga alipombelea na kuzungumza na wanachama wa CCM
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika mkutano huo.