Katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyololo aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kijiji cha Igowole Bw. Josephat Sibadi Soda amerejea CCM baada ya uongozi wa chama hicho kutomlipa madeni ya vifaa mbalimbali alivyochukua madukani wakati wa ujenzi wa mnara wa marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa wakati wa mapambano ya jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA mwaka jana uliojengwa katika kijiji cha Nyololo yeye akiwa mkandarasi na mbunfu wa mnara huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MUFINDI -IRINGA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma mara baada ya kuwasili katika mashamba ya chai ya Ngwazi wilayani Mufindi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi wakishiriki kuchuma chai katika shamba la chai la Ngwazi wilayani Mufindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwagilia maji katika bustani ya miche ya miti ya mbao katika vitalu vya kuotesha miti vya Umoja wa Vikundi vya Kijamii vya Kigamboni mjini Mafinga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda kata ya Nyololo wilayani Mufindi.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili aongee na wananchi wa kata ya Nyololo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa kata ya Nyololo wilayani Mufindi katika mkutano uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda.