Thursday, October 23, 2014

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA AKABIDHI ZAWADI YA BASI DOGO BWAWANI SEKONDARI KATIKA MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA NNE



KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA AKABIDHI ZAWADI YA BASI DOGO BWAWANI SEKONDARI KATIKA MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA NNE
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi funguo za Basi dogo kwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga(kushoto). Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi katika ziara mbambali za Mafunzo hivyo kuondoa kero kubwa ya Usafiri shuleni hapo.
 Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga akijaribisha kuwasha gari jipya lililokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014.
 Muonekano wa Basi dogo lenye Na. MT. 0341 lililokabidhiwa leo Oktoba 22, 2014 na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani. Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari katika ziara mbalimbali za Mafunzo.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(aliyevaa skafu) akiwa meza Kuu amesimama na Viongozi mbalimbali Waalikwa wakati Wahitimu Wakiimba Wimbo Maalum wa Shule katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari leo Oktoba 22, 2014(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula (wa kwanza kulia) ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari leo Oktoba 22, 2014. Jumla ya Wahitimu 95 wametunukiwa cheti cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi Magereza, Mkoani Pwani.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014 Mkoani Pwani.
 Sehemu ya Wahitimu katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne, Bwawani Sekondari wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
 Kikundi cha Wasanii kinachoundwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari kikijiandaa kutumbuiza mbele ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Shule ya Bwawani Sekondari, Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014, Mkoani Pwani.
 Mama mzazi wa Mhitimu wa Kidato cha Nne kutoka familia ya Kifugaji ya Kimasai akimbusu mkono Mtoto wake ambaye amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa na Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014 katika Bwalo la Bwawani Sekondari, Mkoani Pwani
Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).