Zoezi Ushirikiano imara                limefunguliwa leo hii nchini Burundi katika mkoa wa Mwaro,                Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Makamu wa kwanza                wa Rais wa Burundi mhe.Prosper Bazombanza.
        Katika ufunguzi huo mhe                Bazombanza amesema kuwa ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya                Afrika mashariki umetokana na makubaliano ya wakuu wa nchi                wanachama yaliyofanyika mwaka 2001,hivyo kuzitaka nchi                shiriki kuenzi makubaliano hayo kwa kushiriki mara kwa                mara katika mazoezi hayo. 
         Amesema ushiriki katika                mazoezi haya unajenga kujiamini kwa majeshi ya Jumuiya ya                Afrika Mashariki kwa kuwafanya wanajeshi wa Jumuiya hii                kutambua kuwa wapo pamoja katika masuala ya ulinzi.                Gwaride rasmi lilipita mbele ya mgeni rasmi kwa heshma                huku Wakuu wa Majeshi na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya                Afrika Mashariki wakihudhuria sherehe hizo. 
         Kwa upande wa Tanzania                sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa mafunzo wa Jeshi la                Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali James                Mwakibola pamoja na mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali                Venant Mutashobya ambaye kabla ya ufunguzi wa zoezi hili                wakati wote alikuwa akivipokea vikundi kutoka Tanzania                akianzia kupokea kikundi cha JWTZ kilichokwenda Burundi                kwa njia ya barabara katika mpaka wa kabanga na baadaye                kupokea kikundi cha wanamaji wa JWTZ kupitia mpaka wa                Kagunga. 
         Zoezi ushirikiano imara                ni moja ya mazoezi muhimu yanayolifanya Jeshi la Ulinzi la                Wananchi Tanzania kuendelea kuwa moja ya majeshi yenye                weledi wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake                kitaifa na kimataifa. Zoezi hilo linafanyika nchini                Burundi kuanzia tarehe 13 hadi 26 Oct 2014 ambapo                hushirikisha majeshi ya nchi za jumuiya ya afrika                mashariki za Burundi,Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda. 
         Mazoezi ya pamoja kwa                nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yameendelea kufanya                majeshi katika ukanda huu kuwa na weledi kiutendaji hii ni                kutokana na majeshi haya kubadilishana uzoefu katika                Nyanja za kiulinzi na usalama. Wakati huohuo Tanzania                imeteuliwa kuongoza zoezi hilo huku Brigedia Jenerali                Joseph Cosmas Chengelela kuchukuwa jukumu la kuongoza                kombaini ya vikundi vitakavyo shiriki zoezi hilo. 
        Akiongea mara baada ya                ufunguzi, Mkuu wa zoezi kutoka Tanzanina Brigedia Jenerali                Joseph Chengelela amesema ushiriki wa JWTZ katika mazoezi                haya unalifanya JWTZ kuwa miongoni mwa majeshi bora katika                ukanda huu kwani ni njia moja wapo ya kuwafanya maafisa na                askari kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa majeshi                mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
                Brigedia Jenerali Joseph                Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika                Mashariki msaidizi wa zoezi mara baada ya kukabidhiwa                kutoka kwa mgeni rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa                zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI. 
                Meja Jenerali James                Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph                Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini                Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada                ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI. 
                Picha ya Pamoja ya                maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi                ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi                USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI 
                    
              
        .jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
 
