Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe (watano kulia waliosimama) akiwa na                wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya                kukikimbia chao cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).                Wananchama hao 23 wakiongozwa na aliyekuwa Mjumbe wa                Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti                wa Umoja wa Akina Mama wa chama hicho wilayani Nachingwea,                Manufreda Malenga (watano kushoto waliosimama) walifanyiwa                sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo                Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama                hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza                mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Picha                zote na Felix Mwagara. 
                Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM, Mjumbe                wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu                Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia                na Maendeleo (Chadema) wilayani humo, Manufreda Mathias                Malenga. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa                chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na                kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua                ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea                wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili                kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. 
                Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe akimpongeza Mwenyekiti wa Vijana wa                Chadema Kata ya Mtua, Habibu Oswadi (kushoto) baada ya                kukabidhi kadi ya chama chake. Kiongozi huyo wa Kata                pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia                chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa                iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe                alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa                kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya                kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa                Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo na Mwenyekiti wa                Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia                kwa mgeni rasmi). 
                Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya,                Kata pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja uliopo                jirani na Ofisi za CCM Kata ya Mtua katika sherehe kubwa                ya kuwapokea viongozi wawili na wanachama 21 wa Chadema                waliojiunga na CCM wilayani humo. Waziri Chikawe alikuwa                mgeni rasmi ambapo aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi                pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na                upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya                Nachingwea, Regina Chonjo. 
                Mwanachama mpya wa CCM                ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya                Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa                Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani                Nachingwea, Manufreda Mathias Malenga akizungumza kwa                hisia baada ya kupewa nafasi kueleza furaha yake baada ya                kukabidhi kadi ya Chadema na kupewa kadi pamoja na sare za                CCM. Malenga aliwashukuru Viongozi na wanachama wa CCM kwa                kumkaribisha katika chama hicho na kuahidi kutoa                ushirikiano wake ndani ya chama hicho. Kiongozi huyo                pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia                chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa                iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri wa Mambo ya                Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la                Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati meza kuu) alikuwa                mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja                na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na                upinzani wilayani humo. 
        




 
