Na Christian Gideon, Angels moment.
Wanawake wajasiriamali mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza na kuchangamkia fursa zitakazotolewa na kampeni ya mwanamke na uchumi inayotarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi ujao mkoani Tanga ambapo zaidi ya wanawake 300 watanufaika na mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Halima Dendego amesema fursa zitakazotolewa ni fahari kwa wanawake na wajasiriamali wa mkoa huo kwani elimu inahitajika sana wakati huu wa ushindani wa biashara " Fursa kama hizi mara nyingi ni nadra kuzipata na Kampeni ya mwanamke na uchumi ni jibu la changamoto mbalimbali kwa wajasiriamali kwani elimu watakayoitoa ni fursa pekee ya kusonga mbele kibiashara na kiuchumi kwa wanawake wa mkoa wa Tanga" alisema.
Mkuu huyo wa wilaya amewaomba Wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kuunga mkono juhudi za Kampeni ya mwanamke na uchumi kwani kupitia akina mama huduma zao zitaweza kufahamika na kunufaika kwani ndiyo nafasi pekee ya kukutana na wajasiriamali na kusaidia kuinua uchumi wa akinamama na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick amesema kuwa kampeni ya mwanamke na uchumi ni jawabu la changamoto zinazokumba biashara na ujasiriamali kwani elimu na semina zitakazotolewa zitawapa msingi wa kuanza upya kuandaa biashara na ujasiriamali kwa ujumla na pia kutoa hamasa kwa akinamama katika kujiletea maendeleo.
" Kampeni hii inalenga kutoa hamasa na ari kwa akinamama kusonga mbele kimaendeleo, Hakuna ubishi kuwa akinamama wana juhudi kubwa sana za kutafuta fursa za kujiongezea kipato, ila tatizo ni elimu ya msingi ya kuangalia fursa zinazowazunguka na jinsi ya kuendeleza biashara zao."
Angels Moment itawakutanisha akinamama waliofanikiwa kibiashara na ambao wanafanya ujasiriamali mbalimbali ili kuelezana mbinu mbalimbali za mafanikio. Pia kutakuwa na wataalamu watakaotoa elimu ya ujasiriamali, uwekezaji, uwekaji akiba na elimu ya afya' anasisitiza.
Kampeni ya Mwanamke na uchumi Mkoani Tanga itafanyika tarehe tano na sita mwezi ujaokatika Ukumbi wa Naivera ambapo utapambwa na msanii Linah Sanga ambaye ni balozi wa Wanawake.
Wadau walioungamkono kampeni ya mwanamke na uchumi ni MKoani Tanga ni pamoja na SSRA,NSSF,TBS,PSPF,GEPF,AGHAKHAN HOSPITAL,MINJINGUMAZAO,HSC, na NAIVERA COMPLEX .
Mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego akitoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za kampeni ya mwanamke na uchumi Zinazotolewa na kampuni ya Angels Moment ili kumkomboa mwanamke mjasiriamali.
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick {kulia} akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kampeni ya mwanamke na uchumi itakayotolewa tarehe 5 na 6 mwezi ujao mkoani Tanga,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego.