Wednesday, October 15, 2014

BALOZI SEIF AHITIMISHA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUVUMA



BALOZI SEIF AHITIMISHA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUVUMA
Na Othman Khamis Ame.OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaendelea na juhudi zake katika kuona mazao ya wakulima vijijini hasa chakula cha nafaka  yananunuliwa ili kuwaongezea uwezo wa kimapato wakulima hao katika kyukabiliana na ukali wa maisha. 
Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Wananc hi wa Kijiji cha Lugagala kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho pamoja na kuweka jiwe la msingi la nyumba za miradi ya vikundi vya uchumi katika Kijiji cha Muungano Zomba akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za kiuchumi, ustawi wa jamii na maendeleo. 
Alisema Serikali haiwezi kuona nguvu za Wananchi zina potea bure bila ya kuunga mkono hasa ikizingatia kwamba asilimia 90% ya Watanzania wote wanaishi katika maeneo ya uzalishaji vijijini. 
Alifahamisha utafiti na uchunguzi wa kina utafanywa kupitia Halmashauri za Wilaya zinazohusika na uzalishaji wa mazao hayo ya biashara ili kuwadhibiti walanguzi wenye tabia ya kuwanyhonya wakulima kwa ujanja wa kununua mazao yao kwa bei ya chini. 
Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alihimiza kwamba Kiongozi lazima awe mfano wa maendeleo ya jamii badala ya kushabikia vurugu na siasa chafu. 
Mama Asha alisema siasa ni kwa Viongozi kusimamia juhudi na harakati za kiuchumi na maendeleo za wale wanaowaongoza kwa lengo la kuwakomboa kimaisha. Katika kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alichangia Shilingi Milioni 1,500,000/- kusaidia Vikundi hivyo pamoja na kuahidi nguvu za uwezekaji kwa majengo ya vikundi hivyo. 
Balozi Seif pia akachangia shilingi Milioni 1,500,000/- kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Lugagala pamoja na kuahidi kutoa mifuko mia tano ya saruji ya ujenzi wa kituo hicho.
  Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagana na wanavikundi vya uchumi wa Kijiji cha Lugagala wakishangiria ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo katika kijiji pao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la uanzishwaji wa majengo ya vikundi vya uchumi katika kijiji cha Muungano Zomba Mkoani Ruvuma.
 Balozi Seif akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Lugagala kata ya Kilagano Mkoani Ruvuma.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye Mkutano wa Hadhara kwa ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif akiagana na Makamanda wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa ndege wa Songea mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.