Tuesday, October 28, 2014

Airtel yaipeleka Airtel Trace Music Stars Mikoani



Airtel yaipeleka Airtel Trace Music Stars Mikoani
 
 Msanii  chipukizi wa kijiwe cha Matofali jijini Morogoro ajulikanaye kwa jina la Jibwa Kali akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo
 Msanii  chipukizi ajulikanaye kwa jina la Hamisi Ramadhani aka Brashi Waya 2akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo. Pichani ni mashabiki na vijana wa kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro.
Meneja Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando akiongea na wasanii chipukizi wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo.

·         Wasanii chipukizi kutoka morogoro watembelewa katika vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace.

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo.

Akizungumza na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha kuimba  kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.

Mashindano haya yanatoa mwanya wa watanzania wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota kupata fulsa ya kuzifikia ndoto zao. Sambamba na hilo tutakuwa na washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali hapa nchini kama vile pesa taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha washindi wengine toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata nafasi ya nafasi kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani
Nao baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye vijiwe vyao waliweza kushiriki shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia Airtel Trace muziki star huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo itawakomboa wasanii chipukizi wasio na uwezo.

Ambapo Hamis Ramadhan  aka brash waya 2 alikuwa na haya ya kusema" tunashukuru Airtel kwa kutuletea mshindano haya kitaani kwani tunavipaji lakini tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni mdogo tunaamini kwa kuppitia Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na kupigiana kura ili tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea Morogoro na hivyo natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia nafasi hii ili kubuka kuwa masuper star.

Kwa upande wake Ramadhani Nguyao alisema " nimefurahia mpango mkubwa na wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii chipukizi kupata fulsa ya kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi nimevutia na ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi  na wasanii wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.

Mashindano ya Airtel Trace Music Stars yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na October na yatadumu kwa muda wa mienzi sita ambapo fainali ya mashindano haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi 2015 nchini South Afrika.