Sunday, September 14, 2014

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATOA ELIMU YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA WAANDISHI WA HABARI



WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATOA ELIMU YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA WAANDISHI WA HABARI
Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma akifungua Semina ya Waandishi wa Habari kuhusu Magonjwa yasiyoambukiza katika Ukumbi wa Ofisi ya Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Dkt. Ahlam Ali akiwasilisha mada ya maradhi ya Presha katika Semina ya Waandishi wa Habari iliyohusu magonjwa yasiyoambukiza katika Ofisi ya Malaria Zanzibar
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Hassan Vuai akitoa mchango katika Semina ya Waandishi wa Habari kuhusu ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari vya Serikali na Binafsi walioshiriki Semina hiyo wakiwasikiliza watoa mada.
Meneja wa wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Dkt. Omar Mwalimu Omar akitoa ufafanuzi wa masuala yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari katika Semina iliyojadili magonjwa yasiyoambukiza. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.