Monday, September 08, 2014

Waziri wa Viwanda ba Biashara Dr. Kigoda afunga mafunzo ya wajasiliamali zaidi ya 3500 jijini Dar es Salaam



Waziri wa Viwanda ba Biashara Dr. Kigoda afunga mafunzo ya wajasiliamali zaidi ya 3500 jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyoshirikisha zaidi ya wajasiliamali 3500 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Exim Bank Agnes Kaganda baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya tatu kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Badru Idd baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya pili kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa CRDB Albert Michael baada ya benki hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

========  =======  =======

Dar es Salaam. Mafunzo na Kampeni za uhamasishaji nchini Tanzania zitachangia katika kuongeza kasi ya kufanikisha azma ya kutekeleza mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda wakati akifunga Mafunzo ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo iliyoshirikisha wajasiliamali 3,500 kutoka sehemu mbali mbali nchini iliratibiwa na Kampuni ya NUEBRAND na kufadhiliwa na wizara ya viwanda na biashara, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, taasisi ya PESCODE, Tanzania Standard Newspapers, Sayona, Times FM na Kampuni ya Ulinzi ya Kiwango.

Alisema shughuli hizo zinasaidia kusogeza huduma karibu na jamii ya Watanzania ambao wote kwa viwango balimbali ni wawekezaji.
"Wengi wanafikiri wawekezaji ni wakubwa tu.Hapana. Wakulima, wajasiriamali hata wamachinga pia," alisema Waziri Kigoda.

Alisema kuwa muhimu ni kuwa na uongozi unaoratibu shughuli hizo na kuzingatia nidhamu ya kujua uongozi uliopo."Hali hii itapunguza matatizo mengi yanayoendelea sasa kwa wamachinga," alisema Waziri Kigoda.

Aidha,  Dk Kigoda aliongeza akisema wafanyabiashara wote, kwa viwango vyao tofauti wanategemeana kuanzia wamachinga mpaka ngazi ya mitaji mikubwa. Alisema ili kufikia hali hiyo, wawekezaji wa makongamano, mafunzo na kampeni husika ipo haja ya kuendelea kutumia mitandao na mifumo ya teknolojia mbalimbali katika kuelemisha namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa wawekezaji wanaoshiriki katika minyororo ya kuongeza thamani.

"Katika thamani hizo kuna bidhaa za kilimo, ufugaji, madini, misitu, uvuvi hasa vijijini na hata sekta ya huduma inayojumuisha utii, afya na elimu," alisema na kuongeza: "Niwaambieni na kuwafahamisha kuwa moja ya malengo ya Sayansi ni kubuni na kuunda teknolojia na utaratibu wa kufanya kazi zenu ili kutumia mali ghafi na nguvu kidogo, kupata vingi kutoka vichache, kwa manufaa ya taifa."

Ili kuhakikisha tekinolojia inaleta ufanisi, Waziri Kigoda alisema, ni muhimu sana kujikita katika matumizi bora na fursa zinazojitokeza kupitia teknmolojia. "Wito wangu ni kwa taasisi za fedha, na zile za utafiti na sayansi kuendelea kushirikiana na serikali kuona ni jinsi gani tutaendeleza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kupata huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi," alisema.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu nchini wanatumia huduma za fedha za simu, hivyo kama kundi hili likibadilishwa na wakakubali kuwa wateja wa benki nchini, itaongeza upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Nuebrand Events Company, Abdul Ally, akisema kuwa kumekuwa na mafanikia sana toka kampeni hii ianze kwani idadi ya makampuni washiriki yamekuwa yakiongezeka toka 1200 mwaka 2012 mpaka 3600 kwa mwaka huu. "Mafanikio ni makubwa, tumepata pia washiriki toka mikoani mfano Mbeya. Hali hii inatutia moyo," alisema.

Alisema kuwa mwakani uhamasishaji huu utafanyika pia jijini Arusha ikiwa ni katika mkakati wa kuhakikisha mikoa mbalimbali inafikiwa na huduma hii.