Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwakaribisha washiriki wa mafunzo ya wiki 3 ya utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia umuhimu wa matumizi ya takwimu sahihi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15.