Monday, September 08, 2014

TIMU YA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YATUA NANGA KATIKA MIKOA YA SIMIYU NA MWANZA



TIMU YA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YATUA NANGA KATIKA MIKOA YA SIMIYU NA MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Chifu Kishosha Mabiti (wa tatu kutoka kulia) akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (wa pili kutoka kushoto) ramani ya kijiolojia ya mkoa huo mara timu hiyo ilipomtembelea ofisini kwake.
Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Mhe. Mariam Lugaila (mbele kwa mbali) akizungumza na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza zoezi hilo katika wilaya yake.
Afisa Madini Mkazi wa Bariadi Bw. Nyaisara Mgaya ( wa pili kutoka kushoto) akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kulia) moja ya aina ya mawe yenye madini ya ulanga kwenye ofisi za kampuni ya utafutaji wa madini hayo ya African Eagle Resource Ltd.
Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akielezea mchango wa kampuni yake katika ukarabati wa shule ya msingi ya Ntende (inayoonekana pichani) majaji, sekretarieti na wajumbe waliofanya ziara katika shule hiyo.
Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akionesha moja ya kisima kilichochimbwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Ntende mbele ya timu ya majaji na sekretarieti iliyotembelea visima hivyo kama moja ya ufanyaji ya tathmini ya miradi iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa timu ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Mhandisi Moses Ndalahwa (kushoto) akiwahoji vijana wa kijiji cha Ntende kuhusiana na mchango wa makampuni ya madini ya ujenzi katika kijiji hicho.