Wednesday, September 03, 2014

TASWIRA ZA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR Dk.Ali Mohamed Shein visiwa vya samoa


TASWIRA ZA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR Dk.Ali Mohamed Shein visiwa vya samoa
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Kibiashara cha Kimataifa Internationali Trade Center ICT Bibi Arancha Gonzalez walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kibiashara cha Kimataifa International Trade Center,ICT Bibi Arancha Gonzalez akiwa na ujumbe wake jana katika jingo la mkutano wa Tatu wa kimataifa wa nchi za Visiwa.
 Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa makumbusho ya Taifa nchini Samoa Mainifo Viliamu,alipotembelea jana akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwa ziarani huko katika mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Ujumbe wake wakianagalia vitu mbali mbali katika makumbusho ya Taifa la Samoa jana walipotembelea,Rais akiwa huko katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa
 Baadhi ya mabanda ya maonesho ya biashara mbali mbali katika mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa ,mkutano huo wa siku nne unaendelea katika nchi ya Samoa
Baadhi ya mabanda ya maonesho ya biashara mbali mbali katika mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa ,mkutano huo wa siku nne unaendelea katika nchi ya Samoa. Picha na Ramadhan Othman wa IKULU Zanzibar