Tuesday, September 23, 2014

Tanzania Yasisitiza Vipaumbele Vya Kitaifa Vipewe Umuhimu


Tanzania Yasisitiza Vipaumbele Vya Kitaifa Vipewe Umuhumu
Mhe. Waziri Fatma Fereji kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akizungumza kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kikao Maalum cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Jumatatu ambapo wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali kutoka nchi 193 walikutana kutathimini Mpango wa Utekelezaji walioupitisha miaka 20 iliyopita huko Cairo, Misri kuhusu uboreshaji wa maisha ya watu na masuala yahusuyo Idadi ya Watu. Mhe. Fereji ni sehemu ya Ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Fatma Fereji akiwa na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati wa ufunguzi wa Kikao Maalum wa ICPD ambapo Waziri Fereji aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi, Waziri Fatma Fereji wakiwa na Mwakilishi kutoka Ofisi za UNFPA ambaye aliwahi pia kufanya kazi nchini Tanzania akimpongeza Waziri baada ya kutoa mchango wa Tanzania na kulia kabisa ni Dkt. Joyceline Kaganda.