Sunday, September 14, 2014

TANGAZO LA MSIBA WA MZEE IDRISA KILANGI


TANGAZO LA MSIBA WA MZEE IDRISA KILANGI
Bwana Mfaume Kilangi wa Tuangoma Marela-Kigamboni Jijini Dar es Salaam anasikitika kutanga kifo cha baba yake mzazi MZEE IDRISA KILANGI  (pichani) kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wa Marehemu, Mfaume Kilangi Marela Tuangoma jirani na Nyumba za NSSF.

Mwili wa marehemu unataraji kusafirishwa kesho asubuhi saa 3:00 kwenda Iringa mjini kwa Mazishi.


Habari ziwafiukie Ndugu Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mzee Kilangi, popte pale alipo. 

Enzi za Uhai wake Marehemu alikuwa Mkurunzi Mkuu wa Agrofocus, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Korosho Tanzania (CPAT), na pia Rais wa Mpito wa African Cashew Alliance (ACA).