Tuesday, September 23, 2014

Tamasha la 33 la Sanaa lazinduliwa kwa kishindo



Tamasha la 33 la Sanaa lazinduliwa kwa kishindo
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) akifuatilia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael J. Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kati akipiga ngoma kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kulia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw. Ghonche Materego wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii imechorwa sura ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday Richard Kamangu.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kushoto akimpa mkono wa pongezi msanii Sunday Richard Kamangu baada ya kupokea zawadi ya picha iliyochorwa na msanii huyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kushoto, na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi kulia wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani  wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.

Baadhi ya watazamaji wakifurahia mambo yalivyokua wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha zote na: Genofeva Matemu - MAELEZO