Aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Mkakibu wa polisi Ally Mohamed Mkalipa, ambaye ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha, akizungumza wakati wa sherehe ya kuagwa kwake Mirerani juzi.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Mkakibu Msaidi wa polisi, ASP Lwitiko Noman Kibanda, akicheza muziki na mke wake kwenye sherehe ya kukaribishwa kwake na kumuaga aliyekuwa mkuu wa kituo hicho SP Ally Mohamed Mkalipa, ambaye hivi sasa ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, (SACP) Deusdedit Kaizigile Nsimeki, akicheza muziki na mke wake wakati wa tafrija ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa kituo cha Polisi Mirerani Wilayani Simanjiro, SP Ally Mohamed Mkalipa na kumkaribisha Mkuu mpya wa kituo hicho ASP Lwitiko Noman Kibanda.
Wapishi wakiwa tayari kuwahudumia watu mbalimbali walioshiriki kwenye tafrija ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa, ambaye ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha na kumkaribisha Mkuu mpya wa kituo hicho ASP Lwitiko Noman Kibanda.