Familia ya marehemu Stephen E.M Ngereza wa Ilala D'salaam inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa jinsi mlivyoshirikiana bega kwa bega katika kumuuguza mpaka umauti ulipompata ndugu yetu Joyce Stephen katika hospitali ya taifa Muhimbili tarehe 07 septemba 2014 na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 10 Sept 2014 kijijini Maramba Tanga.
Ni wazi kuwa katika kufanikisha kumuuguza mpaka msiba huo mzito mlitumia raslimali zenu kubwa ambazo hazirejesheki kwa namna yoyote ile.
Familia kwa pamoja haina cha kuwalipa kwa moyo wenu wa upendo mliouonyesha zaidi ya kusema neno ahsanteni.
Familia hiyo inawaombea kwa mwenyezi mungu mzidi kubarikiwa na kupewa ziada...Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe...
amen