Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro katika Uwanja wa Ndege wa Comoro leo baada ya kumaliza Ziara ya siku nne kwa mualiko wa Serikali hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Gavana wa Ngazija Mwinyibaraka Said Soilihi (katikati) wakiwa katika mazungumzo na ya pamoja wakiwepo na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi na Mawaziri Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro katika Ofisi ya Gavana huyo jana.