Mpiganaji Danford Mpumilwa, Afisa Habari wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) yenye makazi yake mjini Arusha.akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wa Uganda mjini Kampala kuhusu kazi za mahakama hiyo inayoadhimisha miaka 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mambo ya Nje wa Mahakama hiyo Bocar Sy. ICTR inategemea kumaliza kazi zake hapo mwakani baada ya kuwakamata na kuwahukumu watuhumiwa 83 kati ya 92 waliokuwa wakitafutwa kwa kuhusika na mauaji hayo. Watu 9 bado wanatafutwa.