Mdau Hendrich Nambira au Kenny kama alivyojulikana kwenye mchezo wa kuigiwa wa Mambo hayo katika runinga ITV wakati huo, Alifunga pingu za maisha na mke wake Florence kutoka Visiwani Zanzibar. Harusi ilifanyika katika kanisa la Anglican UMCA, Upanga jijini Dar es Salaam tarehe 23/08/2014.
Mama Bishanga na mumewe hawakuweza kuwahi siku ya harusi hiyo iliyopendeza sana na kuhudhuriwa na ndugu wengine wakiwemo wadogo wa mama Bishanga Mack Innocent Hatia na Constancia Innocent Hatia, baba mkubwa mzee John Kamota na shangazi Rehema Kamota, bibi wa Kenny mwalimu Agnes Innocent Hatia na ndugu zetu wengine, pia marafiki na wawakilishi wa wasanii toka Bongo movie. Sherehe ya kukata na shoka ilifanyika Lion Hotel.
Bwana harusi Kenny na mkewe Florence wakiwa pwani Oster Bay mara baada kumeremeta kwao.
Maharusi wakikata keki ya harusi yao
Kaka wa bwana harusi Kilian Kamota na mama yao mdogo Fridah Mchauru wakipiga cheers ya shampein .
Dada wa bwana harusi Sizelina ambae ni mtoto wa kwanza wa mama Bishanga akilisakata rumba kwa raha na furaha tele ya harusi ya mdogo wake.