Friday, September 26, 2014

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) yakamilisha kituo cha kupokea na kutuma mawasiliano ya Ndege



Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) yakamilisha kituo cha kupokea na kutuma mawasiliano ya Ndege
Mhandishi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Valentine Kayombo akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo pichani) faida zitakazopatikana kutokana na kukamilika kwa Kituo hicho ikiwamo kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka Hiyo Bi. Bestina Magutu. 
Inspeka Mwandamizi Idara ya Udhibiti Usalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Redemptus Bugumula akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ongezeko la marubani wanawake nchini ambao wanafikia Takribani Kumi kwa sasa wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi.Valentine Kayombo.

  Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa maboresho ya kituo cha Mawasiliano ya Radio kwa ajili ya usafiri wa anga kilichopo Mnyusi mkoani Tanga, kilichojengwa na kampuni ya JATRON ya Norway, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi. Valentine Kayombo.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.