Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
Baadhi ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.