Wednesday, September 17, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO KATI YA VYOMBO VYA HABARI NA VYOMBO VYA ULINZI, USALAMA NA SHERIA, JIJINI DAR


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO KATI YA VYOMBO VYA HABARI NA VYOMBO VYA ULINZI, USALAMA NA SHERIA, JIJINI DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa Mashauriano kati ya Vyombo vya Habari na Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2014. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Rais wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Jaji Thomas Mihayo, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi Mukajanga, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.