Thursday, September 18, 2014

KUMBUKUMBU YA MIAKA 7 YA KIFO CHA MZEE SHAURI TIMOTHEO NATHAN



KUMBUKUMBU YA MIAKA 7 YA KIFO CHA MZEE SHAURI TIMOTHEO NATHAN


Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007)
  
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika saba sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/08/2025. 

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki "Father Kidevu".

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.

Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Imanuel Kajiru, Elizabeth Kajiru, Timothy Kille, Maria Thomas, Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan Dossa, Dinner Onesmo,Digna Onesmo, Debora Daniel na  Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani, Kidai na Shauri.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana pamoja na wote wa Ugweno, Kilimanjaro.

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa "TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE," baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.