Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew Chenge (mjumbe) akiongoza kikao cha kamati hiyo jana ambapo kamati hiyo inamalizia uandishi wa Katiba pendekeze inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Jumatatu wiki hii. Kamati hiyo inachambua maoni ya taarifa za Kamati pamoja na michango ya Wajumbe wakati wa Mjadala na kuyaweka maoni hayo pamoja na kisha kuandaa katiba inayopendekezwa. picha na Owen Mwandumbya.