Tuesday, August 19, 2014

Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii akabidhi tuzo na kutembelea Hospitali ya Rufaa kanda ya Kati singida



Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii akabidhi tuzo na kutembelea Hospitali ya Rufaa kanda ya Kati singida
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(mb), amehudhuria hafla ya utoaji tuzo kwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida.tuzo hiyo inahusiana na mafanikio yaliyokwisha na hospitali hii katika kuinga na kudhibiti maambukizi kutoka kwa magonjwa Kwenda kwa mtoa huduma na vile vile kutoka kwa mtoa huduma Kwenda kwa magonjwa.mradi huu unasimamiwa na wizara ya Afya na ustawi wa Jamii chini ya ufadhili wa mashirika ya kimarekani ambayo ni PEPFAR, JHPIEGHO na CDC. Tuzo hiyo hutolewa kwa hospitali au Kituo cha kutolea huduma za Afya baada ya kuikodi vigezo na kupata alama kuanzia asilimia 80 na kuendelea ya vigezo vinavyotumika katika kutathmini utekelezaji wa programme hiyo.