Tuesday, August 19, 2014

MH. PINDA KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA JUKWAA LA KILIMO



MH. PINDA KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA JUKWAA LA KILIMO
Katibu Mtendaji Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa  Jukwaa la Wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka litakalofanyika Agosti 20 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo na Ofisa Programu wa Women & Youth Development Foundation, Luke Daniel Kifyasi.
Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo  akizungumza wakati wa mkutano huo.
Na Clezencia Tryphone

Waziri Mkuu Pinda, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara baada ya kuvunwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge amesema katika uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip Agosti 20 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi.
Alisema lengo la kufanya uzinduzi huu ni kutokana na changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
 
Miongoni mwa changamoto hizo, ni utuzwaji wa mazao hayo baada ya kuvunwa, hasa kwa wakulima wadogo wadogo na wale wa kati na wafanya biashara huku changamoto nyingine ikiwa ni upotevu wa Mbegu pamoja na matumizi ya tekinolojia ya utunzaji na takwimu.

"Tunatarajia kufanya uzinduzi wa jukwaa la wadau wanaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara tu baada ya kuvuna, na lengo kubwa ni kuwaamasisha pia watunzaji wa nafaka hizo, ili kuepuka upotevu, na tumefikia hatua hii baada ya kufanya utafiti,"amesema Rukonge.

Amesema, mara baada ya kufanywa kwa takwimu wamegundua kuwepo kwa upotevu mkubwa wa mbegu za mazao hayo na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.