Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu Kayandabila akionyesha mbegu za mahindi zilizohifadhiwa kwenye ghala aina ya Silo, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu Kayandabila akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
Mmoja wa wadau wa kilimo akichangia mada katika uzinduzi wa jukwaa la kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa. Ghala la kuhifadhia chakula aina ya Silo.
SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika imekili uwepo wa tatizo la upotevu wa mazao hasa jamii ya Mikunde na Nafaka ambalo ni tatizo kubwa, linalowakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la wadau watakaoangalia mazao mara baada ya kuvunwa jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Yamungu Kayandabila alisema, hata wizara yake inalitambua suala hilo, na imeanza harakati za kupambana na janga hilo, hasa kwa kuwaamasisha wakulima na wauzaji kutunza mazao hayo katika maghara.
"Tatizo la upotevu wa mazao ni tatizo kubwa, na hilo linachangiwa na uhifadhi duni ambapo zaidi ya asilimia 30 utokea katika upotevu wa mazao hayo,"alisema Kayandabila.
Kayandabila ambaye alikuwa mgeni rasm katika uzinduzi wa jukwaa hilo ulioandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Ansaf, aliipongeza taasisi hiyo kwa jitihada ambazo wanazionyesha katika kukomesha tatizo hilo, huku pia akiyataka mashirika, taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Ansaf.
"Tunawashukuru sana Ansaf kwa kufanya uzinduzi huu, na naimani taasisi na mashirika mengine yatafuata nyayo zao katika kutokomeza suala hili la upotevu ili wakulima na wafanya biashara waweze kuzihifadhi vizuri,"alisema Kuyandabila na kusema kuwa Serikali pekee haiwezi bila ya sapoti ya watu kama wao.
Naye Katibu Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge alisema, wamegundua changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanya biashara kwa ujumla na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.
Naye mmoja wa wajumbe walioudhulia uzinduzi huo, Lusekelo Mwandemange ambaye ni mkulima wa zao la Mpunga kutoka Kyera, alisema, amefarijika kupata nafasi hiyo, huku akiwataka Ansaf kuhakikisha wanatoa elimu zaidi kwa wakulima walioko Mikoa mbalimbali.