Kinamama wa kundi la ngoma za utamaduni la Simba kutoka kijiji cha Nhambi, Wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma wakitumbuiza kwa ngoma ya Kigogo huku wakiwa wamekula uzi wa Man U wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa maji uliofanywa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 29, 2014 katika kijiji cha Chunyu.