Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo, Martha Sengeruan.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya Sayansi wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia vitabu hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.
Meijo alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Aidha alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa kutoa mifugo yao.
"Changamoto kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji na umeme wa kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa mitihani yao kwa kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa wanafunzi hao" alisema Meijo.
Ameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka ilikuweza kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia kusaidiwa upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa msaada huo wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa ufaulu shuleni hapo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al Amin.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na Wizara ya Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu wenu kama wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika ujenzi wa taifa.
Bw. Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule hiyo kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa ajili ya masomo.
Shule hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana ya Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba hiyo kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla ya kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa "Software" ya kisasa zaidi na kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na Mwalimu wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) na fisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y sekondari ya wasichana MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi shuleni hapo Bw. Edickiel Mturi.
Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu shuleni hapo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu.