Kina mama                wakionyesha mfano wa kuwanyonyesha watoto wachanga katika                kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani                yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa 
                 Baadhi ya                wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya                Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani                Mufundi mkoani Iringa.
                 mwakilishi                wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa                (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards akizungumza. (picha                zote na Denis Mlowe)
                 Katibu Mkuu                wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo                akizundua kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya                Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo katika kilele cha                maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika                kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto) ni                kaimu mkurugenzi wa mtendaji wa taasisi ya chakula na                lishe tanzania Dk. Joyceline Kaganda na katibu tawala mkoa                wa Iringa Wamoja Ayubu.
                 Katibu Mkuu                wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo                akionyesha kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya                Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo mara baada ya                kukizundua rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya                Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani                Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto)ni katabu tawala mkoa                wa Iringa na kulia nimwakilishi wa Unisef tanzania Paul                Edwards.
         Wanajeshi                wa KJ Mafinga wakiigiza kuhusu janga la Ukimwi katika wiki                ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani                Mufundi mkoani Iringa.
                 Wanajeshi                wa KJ Mafinga wakiimba kwa hisia kali kuhusu janga la                Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika                kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
         Baadhi ya                wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya                Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani                Mufundi mkoani Iringa.
                 Msanii wa marufu nchi Emanuel Mgaya              'Masanja' akiongoza maandamano ya kuadhimisha kilele cha               maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika              kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi.Na Denis Mlowe,Mufindi. 
        SERIKALI imewataka waajiri katika taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia na kulinda sheria zinazowalinda wanawake wanaojifungua kwa kuwapa likizo za uzazi kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake.
Akizungumza katika kilele cha                  maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani                  yaliyofanyika kitaifa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa                  juzi, mgeni rasmi Katibu wa Mkuu Wizara ya Afya na                  Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo, mwanamke                  aliyejifungua mtoto mmoja anatakiwa kupewa likizo ya                  uzazi ya siku 84 na aliyejifungua watoto mapacha anapewa                  likizo ya siku 100.
        Alisema likizo hizo                  zinaambata na malipo kamili ya mshahara na mama                  aliyejifungua anaweza kuchukua likizo yake ya mwaka                  akihitaji na mzazi aliyerudi kazini baada ya likizo ya                  uzazi anapewa ruhusa ya saa mbili kwa siku kwenda                  kumnyonyesha mtoto.
        Pallangyo aliwaasa wadau                  wengine wanaojishughulisha na uuzaji wa maziwa mbadala                  ya watoto, mikoa na halmashauri zote kujua na kufuata                  kanuni za kitaifa zilizotungwa chini ya sheria za                  mamlaka ya chakula dawa na vipodozi sura ya 219                  kudhibiti uuzaji na usambazaji wa maziwa mbadala ya                  watoto pamoja na bidhaa zinazoambatana na vyakula vya                  watoto.
        Aidha alivitaka vyombo vya                  habari kuelimisha wanafamilia na wanawake hasa wanawake                  wanaojiita wa kileo ambao wanaiga tamaduni za kigeni za                  ulishaji watoto ambazo mazingira yake ni potofu.
        "Tungependa kuwaona hawa                  wanawake wa kisasa wanabadilika na kuelewa kuhusu                  umuhimu wa kunyonyesha watoto hasa katika miezi sita ya                  mwanzo ili kuwajengea watoto msingi mzuri kimwilina                  kiakili hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau                  mbalimbali zikiwemo kamati za lishe za mikoa na wilaya                  ili kuhakikisha kwamba elimu inatolewa kwa wanawake                  wote" alisema Pallangyo 
        Awali Mkuu wa mkoa wa Iringa                  Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa na                  Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Ayubu Warioba, aliitaka                  jamii kuelimishana kwenye kaya na jamii kuhusu                  unyonyeshaji na ulishaji sahihi wa watoto katika ustawi                  na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
        Alisema jukumu la kuboresha                  afya na uhai watoto wa kitanzania ni la wananchi wote                  likianzia na mtu binafsi na familia kwa ujumla.
        Kwa upande wake mwakilishi wa                  shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF)                  nchini Tanzania  Paul Edwards alisema shirika hilo na                  wadau wengine linalenga kuimarisha unyonyeshaji  wa                  maziwa ya mama kama njia ya ufanisi na kuokoa maisha ya                  mtoto.
        Alisema shirika hilo                  litawajengea uwezo watoa huduma za afya kwenye vituo na                  wahudumu wa afya vijijini pamoja na watu wengine ambao                  ni muhimu katika kufanikisha mipango ya kuboresha lishe                  kwa watoto
                          
