Mkuu wa wilaya                ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa                maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa                Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al                Amin Yusuph (wa tatu kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo                wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania , Bw. Slyvester                Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ubalozi                wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na                mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick                Ndoinyo (kushoto kwa DC).
        Na                Mwandishi wetu, Ngorongoro
        Serikali                na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa                ushirikiano kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo                la kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wao.
        Hayo                yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM,                Joseph Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi                inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni                (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi                inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na                wadau wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa                Uswiss hapa nchini.
        'Redio                za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na                jamii katika suala zima la kujiletea maendeleo' alisema                Joseph Munga.
                Mkuu wa wilaya                ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na                wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi                ya maendeleo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi                na Utamaduni (UNESCO).
        Munga                aliongeza kwa kusema kuwa redio hiyo iliyoanza kurusha                matangazo mwezi Oktoba 2013 imekuwa ni kichocheo cha kutoa                taarifa mbali mbali kwa jamii wilayani Loliondo na kuibua                changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii huku akiitaka                serikali na halmashauri wilayani humo kuisaidia katika                kufikia malengo ya kuitumikia jamii na kuwashukuru wadau                mbali mbali wanaoiwezesha redio hiyo ikiwemo kampuni ya                simu za mkononi ya Airtel ambayo imetoa mnara wao kurushia                Matangazo ya redio Loliondo.
        "Suala                hapa ni ushirikiano hasa kwa halmashauri kuelewa na kuona                umuhimu wa kutumia redio hii katika matukio mbali mbali                yanayofanyika kwenye halmshauri vikiwemo vikao vya baraza                la madiwani ili wananchi walioshindwa kufika waweze kujua                baraza lao limepitisha nini sanjari na huduma kwenye sekta                za afya na elimu", alisema Munga.
        Redio                Loliondo ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO                wilayani humo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya                RAMAT kwa kufadhili miradi ya Maktaba,kutoa elimu kwa                jamii ya kifugaji yenye malengo ya kuinua uelewa na                ufahamu kwa jamii hizo zilizopo pembezoni hasa katika                suala zima la kujiletea maendeleo.
                Afisa Miradi ya                Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin                Yusuph (kushoto) ambaye pia ndio mkuu wa msafara huo                akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,                Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo hayo. Kulia ni Meneja                Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester                Nteere.
        Nae                Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO,                Bw. Al Amin Yusuph, alisema kuwa misingi ya redio hiyo                inalenga kuikomboa jamii ya Loliondo kwa kutoa elimu ya                kifugaji na elimu kwa wananchi wilayani humo ambao hapo                awali hawakupata fursa ya kupata taarifa na matukio                mbalimbali yanayoendelea wilayani humo. 
        Akifafanua                faida za redio hiyo kwa jamii ni kupata taarifa mbali                mbali zinazoendana na shughuli zao za ufugaji hususan                taarifa za chanjo ya mifugo na madawa na kupata taarifa                nyingine kuhusiana na masuala mbali mbali ya kijamii ndani                na nje ya wilaya hiyo ambayo hapo awali yalikuwa vigumu                kupatikana kwa wakati kutokana na jiografia ya wilaya                hiyo.
        "Pamoja                na kwamba malengo ya mradi huu yameanza kuonekana dhahiri                machoni petu,wafadhili kutoka UNESCO pamoja na kampuni ya                simu za mikononi ya Airtel ambayo mnara wake umekuwa                ukitumika kurusha matangazo ya redio hii, tunataka                kuhakikisha kwamba mnaweza kujiendesha wenyewe hapo baadae                ili mradi kama huu uweze kuwanufaisha na wenzenu sehemu                zingine", alisema Al Amin.
        Akizungumzia                miradi inayoletwa na wafadhili wilayani humo Mkuu wa                wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa                imechangia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha vijana ambao                wana shauku ya kuishi mijini kurudi nyumbani na kuendeleza                jamii hali ambayo imetafsiriwa kutoa uelewa kwa wanajamii                na hivyo ni faraja kubwa kwa wananchi wilayani Loliondo.
        Ameyataka                mashirika na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali                kuingalia Ngorongoro kwa ukaribu na kuwa wadau wazuri wa                kuiletea maendeleo wilaya hiyo kwani miradi iliyopo                itachochea ukuaji wa uchumi na kusaidia uelewa wa wakazi                wilayani Loliondo katika dhana nzima ya kujileta maendeleo                na kukuza uelewa wa wananchi wa kupata taarifa mbalimbali                kwa wakati.
                Afisa Miradi ya                Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin                Yusuph (wa pili lulia) akitoa ushauri kuhusu kituo hicho                kuwa kitakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa jamii hiyo ya                kifugaji pindi kitapokamilika huku akisisitiza kuwa                mipango iliyopangwa kama walivyopewa maelezo iendane na                wakati.
                Mmoja wa wadau                wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick                Kalunga akisoma moja ya vitabu ndani ya maktaba hiyo                inayofadhiliwa na UNESCO, Maktaba hiyo inayotumiwa na                wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa                kata hiyo.
                Afisa Miradi ya                Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin                Yusuph (kulia) ambaye pia ni mkuu wa msafara huo wa                kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO akiteta jambo na                Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester                Nteere ndani ya maktaba hiyo. Anayefuatilia mazungumzo                hayo kwa karibu ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani                ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na                mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (katikati).
                Afisa Miradi ya                Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin                Yusuph (wa pili kulia) akitoa maelezo baada ya kutembelea                Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO nje ya maktaba hiyo.
                Kikundi cha                ngoma ya Kimasai kilichowatumbuiza wageni waliotembelea                mradi wa redio ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO                wakitumbuiza wakati wa ziara hiyo.
                Afisa Miradi wa                kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko,                akijumuika na kinamama wa kikundi cha ngoma za kimasai                kutoka kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani                Arusha.
                Diwani wa kata                ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika                lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo                FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya                miradi mbalimbali ikiwemo maktaba, redio na ugawaji wa                vitabu vya masomo ya Sayansi na hesabu vinavyoafadhiliwa                na UNESCO kwenye kata hiyo.
                Meneja Mauzo wa                Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akitoa                pongezi kwa redio Loliondo FM kwa kuweza kuihamasisha                jamii inayoizunguka kwa kuburudisha, kutoa elimu na habari                kwa ujumla hiyo sio kazi nyepesi kutokana na uchanga wenu                wa redio yenu.
                Meneja Mauzo wa                Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akikabidhi                zawadi kwa kikundi cha ngoma cha kinamama wakati wa ziara                hiyo ya ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na UNESCO kwenye                kata ya Ololosokwani.
                Wanakikundi cha                ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia                taarifa mbalimbali za mitandao kwenye "Tablet"                inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara                hiyo.
                Mmoja wa                wanakikundi akitumia Tablet kupiga picha wanakikundi                wenzake pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani).
                Wanakikundi cha                ngoma za kimasai wakiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni                huo huku wakionyesha furaha baada ya kupokea zawadi ya                fulana kutoka kampuni ya Samsung.
                Meneja wa redio                jamii ya Loliondo FM, Joseph Munga akiwa kwenye studio za                redio hiyo wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi                inayoifadhili.
                Meneja mauzo wa                Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (aliyeketi)                akiwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa                UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph ndani ya studio za kurushia                matangazo za redio ya Loliondo FM inayorusha matangazo                yake kwenye mnara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel                na kuifika jamii kubwa kwenye maeneo hayo.
         
