Sunday, August 31, 2014

MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA WAZIRI WA AFYA NA WAZIRI WA MIUNDOMBINU ZNZ


MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA WAZIRI WA AFYA NA WAZIRI WA MIUNDOMBINU ZNZ
1Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Waizara ya Afya Juma Rajab Juma kulia akiwakaribisha Mawaziri wa Afya na Miundombinu katika hafla ya kukabidhiana Ofisi mawaziri hao baada ya kuteuliwa katika nafasi zao hivi karibuni.
2Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Afya katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.3Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akimkabidhi Ripoti Waziri mpya wa Wizara ya Afya Rashid Seif Suleiman katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.4Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Juma Duni Haji.