Wednesday, August 13, 2014

MAGUFULI AKAGUA MIZANI YA KISASA YA VIGWAZA MKOANI PWANI PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA KIBAMBA-KWEMBE-MAKONDEKO (17KM) ITAKAYOPITA KATIKA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI, MLOGANZILA, KIBAMBA


MAGUFULI AKAGUA MIZANI YA KISASA YA VIGWAZA MKOANI PWANI PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA KIBAMBA-KWEMBE-MAKONDEKO (17KM) ITAKAYOPITA KATIKA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI, MLOGANZILA, KIBAMBA
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliyevaa kofia akipita juu ya Mzani mpya  wa Vigwaza Mkoani Pwani  ambao ni wa kwanza na wakisasa zaidi kujengwa nchini Tanzania  ambao utaruhusu magari kupima bila kusimama hivyo kuondoa malalamiko kutoka kwa wasafirishaji.
 Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Ndugu Kileo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli jinsi Mzani mpya wa Vigwaza utakavokuwa ukipima magari wakati yakitembea tofauti na mizani mingine nchini.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Mzani mpya uliopo Vigwaza Mkoani Pwani ambao unapima magari wakati yakitembea.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusu Mzani mpya unaopima magari wakati yakitembea Vigwaza mkoani Pwani
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya ujenzi  inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo katika eneo la Mloganzila Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Dkt. Magufuli alipita hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wa Kibamba mara baada ya kufanya mkutano kuhusu mradi wa ujenzi wa wa  barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Wakanadarasi wakati wa ziara yake yakutembelea na kukagua ujenzi wa   barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kibamba kuhusu ujenzi wa   barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Taaswira ya Mzani mpya wa Vigwaza kama unavyoonekana
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Julius Ndyamukama kuhusu ujenzi wa Barabara ya kiwango cha Lami kutoka Kibamba-Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilomita 17