Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda (wa pili kushoto) akifungua Mafunzo ya uwezeshaji kuhusu mabadiliko ya Tabianchi na athari zake kwa walimu wa somo la Jiografia kutoka Manispaa ya Kinondoni. Kushoto ni kiongozi wa walimu wanaopata mafunzo Mwl. Nesta Mwamfupe. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Walimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza muwezeshaji wakati wa mafunzo ya uwezeshaji kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa walimu wa Jiografia, mafunzo yanaratibiwa na Kituoa cha Mafunzo ya Tabianchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kielelezo cha mafunzo kuhusu ongezeko la gesi joto duniani.