Tuesday, August 26, 2014

KURA HAZIKUTOSHA KWA ROSE, SHUSHO NA GAZUKO TUJIPANGE MWAKANI


KURA HAZIKUTOSHA KWA ROSE, SHUSHO NA GAZUKO TUJIPANGE MWAKANI
Waandaaji wa tuzo hizo wakiwa na wageni waalikwa Zanele Mbokazi na mumewe waandaji wa tuzo maarufu za injili za Crown za nchini Afrika ya kusini.

Hatimaye tuzo za injili za Africa gospel music awards kwa mwaka 2014 zilitolewa usiku wa jumapili hii huko jijini London nchini Uingereza na kushuhudia waimbaji watatu kutoka nchini Tanzania ambao walipendekezwa kuwania tuzo hizo wakitoka mikono mitupu.

Tuzo hizo ambazo zilikuwa zikifanyika kwa mara ya tano, ni waimbaji wa nchi jirani ya Kenya ndio waliondoka na tuzo kwa mwaka huu pamoja na waimbaji wengine kutoka barani Afrika hususani Afrika magharibi, Ghana na Nigeria. Katika tuzo hizo Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na waimbaji watatu Rose Muhando aliyekuwa akiwania tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa mwaka barani Afrika tuzo ambayo imetwaliwa na wadada wawili Diana Hamilton pamoja na Nikki Laoye.

Aidha kwa upande wa Christina Shusho aliyekuwa akiwania tuzo mbili ikiwemo ya video bora ya mwaka kupitia wimbo wake wa Nataka nimjue, tuzo hiyo imechukuliwa na Sammy Okposo wa Nigeria kupitia wimbo wake wa 'Who tell you say', huku tuzo ya mwimbaji bora wa Afrika mashariki ikichukuliwa na mwanakaka Bahati kutoka nchini Kenya.

Aidha kwa mara ya kwanza mwimbaji wa muziki wa kufokafoka ama rap za injili Gazuko Junior aliyeandika historia ya kuwa mwimbaji wa kwanza wa mtindo huo kutoka nchini kuingia katika tuzo hizo hakuweza kuipata tuzo hiyo ambayo ilichukuliwa na Miller Luwoye wa Uingereza. GK inawapongeza waimbaji wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo kwakuwa hiyo ni hatua kubwa sana ambayo inaonyesha muziki wao na huduma yao kutambuliwa kimataifa, pia kwa wapigaji kura itabidi tuongeze juhudi mara dufu mwakani ili kura zitoshe na hatimaye tuzo hizo zije Tanzania.

Mungu awabariki sana, ukitaka kuona orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo bonyeza HAPA.

                             Mtazame Sammy Okposo na video yake iliyochukua tuzo