Tuesday, August 12, 2014

KAMPUNI YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA SHINDANO LA MASHAMBA DARASA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.



KAMPUNI YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA SHINDANO LA MASHAMBA DARASA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.
Kampuni ya Seed Co Tz Ltd imezindua rasmi shindano la mashamba darasa kwa shule za Msingi Tanzania ambapo shule itakayokuwa imelima shamba zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15 za Kitanzania. 
Tunaposema kulima kwa kuzingatia misingi ya kilimo bora cha kisasa ni pamoja na matumizi ya mbegu bora, mbolea za kupandia na kukuzia na uhifadhi bora wa mazao baada ya kuvuna. Shindano hili ni mahsusi kwa shule za msingi zilizopo katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Kagera, Kigoma, Tabora, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara. 
 Hii ni baada ya kugundua kuwa ukiachia mbali juhudi za serikali katika kukifanya kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu, changamoto kubwa bado imebaki kuwa katika elimu ya somo hili. 
Na ndio maana kampuni ya Seed Co ikaona kuwa kama tunataka kufikia malengo haya basi juhudi kubwa inatakiwa iwe katika kufundisha Watanzania kilimo kwa njia ya vitendo kwa kuanza kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na kuwapa motisha ya kujishindia zawadi kemkem kutoka Seed Co. 
 Ukiachia mbali zawadi kuu ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15 za Kitanzania, zawadi nyingine zitakuwa ni sare za michezo, vibao vya kuandikia, madaftari na kalamu za kuandikia. Bila kusahau kuwa mwalimu wa somo la kilimo ambaye ataifanya shule yake ishinde atazawadiwa pia simu ya kisasa ya mkononi. 
 Ili kushiriki, wanafunzi au walimu wanatakiwa kutembelea maduka ya mawakala waliothibitishwa wanaouza mbegu za Seed Co au kununua gazeti la Nipashe toleo la kesho tarehe 13 Agosti 2014 ambapo watajipatia nakala yenye tangazo au fomu ya kujiunga na shindano hili. Kumbuka mwisho wa kujisajili kwa shindano hili ni tarehe 30 mwezi Agosti 2014. 
 Katika uandaaji na usimamizi wa mashamba darasa haya, kampuni ya Seed Co itatoa pembejeo zote zinazohitajika, ikiwa ni mbegu za mahindi, mbolea ya kupandia na kukuzia na pia madawa ya kupulizia iwapo mazao yataonyesha dalili za kushambuliwa na wadudu waharibifu. Kumbuka ya kwamba kampeni hii ya Mashindano ya Mashamba Darasa imelenga kufundisha Kilimo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, huku ikitoa nafasi kwa wanafunzi kujishindia zawadi mbali mbali kutoka Seed Co. Zawadi kuu ni kushinda Madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 15 za Kitanzania.
Hii ni motisha kubwa kwa wanafunzi kupenda shughuli za kilimo tangu wakiwa shuleni. Kuhusu Seed Co Seed Co Limited ni kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kukuza, kuzalisha, kubangua na kusambaza mbegu bora katika masoko ya nchi 15 barani Afrika. 
Bidhaa nyingi za mbegu zinazozalishwa na kampuni hii ni pamoja na mahindi, Pamba, Ngano, Soya, Mtama na mazao mengine ya nafaka ndogondogo.
 Katika soko la Tanzania Seed Co imejikita zaidi katika uzalishaji wa mbegu chotara za mahindi na mtama. Kampuni hii kwa sasa ina viwanda vya kubangua mbegu Jijini Arusha na Mbeya. Jijini Mwanza kuna ghala kubwa la kuhifadhia mbegu ikiwa ni mkakati wa kumfikishia mkulima bidhaa hizi karibu naye.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbegu ya Seed Co ya jijini Arusha,Frank Wenga(kulia)akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari leo,kushoto ni Meneja Mauzo,Daniel Mwambugi.
Meneja Mauzo wa  Kampuni ya Mbegu ya Seed Co ya jijini Arusha,Daniel Mwambugi(kushoto) na Meneja Masoko,Frank Wenga wakionesha Fomu maalumu itakayotumiwa na wanafunzi wa Kanda ya Ziwa kushiriki shindano hilo.