Friday, August 29, 2014

JWTZ LATOA MSAADA KWA WAZEE NA MAYATIMA ZANZIBAR



JWTZ LATOA MSAADA KWA WAZEE NA MAYATIMA ZANZIBAR
MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akizungumza na Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee Sebleni mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya usafi vilivyotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964.
WAZEE wanaoishi katika nyumba za wazee Sebleni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza katika makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo.
KAIMU Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Kanali Shaban Ilangu Lissu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi vilivyotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)kwa Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee Sebleni ikiwa ni kutimiza miaka 50 ya kuanzishwa kwa JWTZ.Kulia Naibu Katibu Mkuu Uwezeshaji na Ushirika, Nd. Ali Khamis .
MASISTA wanaowalea wazee wanaoishi katika nyumba za wazee welezo wakiwa katika hafla ya kumakabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya Jeshi hilo ambapo misaada kama hiyo ilitolewa kwa Tanzania nzima kwa wazee wasiojiweza na mayatima.
WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishusha msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi vilivyotolewa na jeshi hilo kwa Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee ziliopo Welezo Wilaya ya Magharib.Kushoto anaeshughudia Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Kanali Shaban Ilangu Lissu.
MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akiwakabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya kufanyia usafi Watoto yatima wanaoishi katika nyumba za mayatima Mazizini. Msaada huo ulitolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika kutimiza miaka 50 ya kuanzishwa kwake.
MKUU wa Mkoa Mjini Magharib, Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika nyumba za mazizini, baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula vilivyotolewa na JWTZ katika kutimiza miaka 50 ya jeshi hilo.(Picha na Haroub Hussein).