Tuesday, July 29, 2014

WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)




WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)
 Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini. 
  Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam
 

 Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha moja ya tuzo waliyotunukiwa Tanzania na Baraza la Usafiri wa Anga Duniani kwa kutambua mchango wa TCAA. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mweneyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt.Weggoro Nyamajeje,  wakati alipofanya ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.