Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO), Luteni Generali Sebastian Ndeitunga (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) kuhusiana na utekelezaji wa maazimio ya SARPCCO. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO), Luteni Generali Sebastian Ndeitunga (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) kuhusiana na utekelezaji wa maazimio ya SARPCCO. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, na wapili Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Issaya Mngulu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO), Luteni Generali Sebastian Ndeitunga (kulia) kuhusiana na utekelezaji wa maazimio ya SARPCCO. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
…………………………………………………….
Na Immaculate Makilika na Winner Abraham-MAELEZO
WANANCHI wa Nchi za Kusini mwa Afrika wametakiwa kushirikiana na Majeshi ya Polisi ili kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu yanayozikabili nchi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Namibia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Polisi wa Nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Luteni Jenarali Sebastian Ndeitunga kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Luteni Jenarali Ndeitunga ameongeza kuwa ni vyema wanajamii wakawa mstari wa mbele kutoa taarifa kwa Polisi endapo kuna mashaka katika shughuli zozote zinazoendelea katika maeneo yao ambazo zina hisia ya kusababisha uhalifu wa aina yoyote.
Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia vikosi vya Polisi kudhibiti kwa haraka uhalifu kabla haujaleta madhara makubwa kwa jamii na kurudisha nyuma maendeleo.
Mkuu huyo amesema kuwa baadhi ya uhalifu ambao umekuwa ukifanyika katika Nchi zilizopo kwenye Umoja wa SARPCCO ni pamoja na ugaidi ,usafirishaji wa dawa za kulevya na binadamu.
Hata hivyo, Luteni Genarali Ndeitunga amesema SARPCCO kwa kushirikiana na INTERPOL imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali,ikiwemo kufungua mashitaka kwa watuhumiwa,na kurudisha mali zilizoibiwa kwa wahusika.
Ameongeza kuwa pamoja na jitihada mbalimbali za kukabiliana na uhalifu huo, SARPCCO inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kisasa ambavyo husaidia kubaini uhalifu kwa urahisi.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amesema Serikali inaendelea na Uchunguzi kufuatia milipuko ya mabomu iliyotokea jijini Arusha hivi karibuni na kuiomba jamii kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kukomesha matukio ya uhalifu yanayoendelea kujitokeza Nchini.