.Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Abraham Nyanda akisoma hotuba yake wakati wa kufunga Mafunzo Unganishi(Bridging Course)yatakayowawezesha kujiunga na mafunzo ya Stashahada ya Uandisi,kushoto ni Mtaalam wa Umwagiliaji kutoka Japan,Nobuyoshi Fujiwara na Mkuu wa Chuo,Dk Richard Masika.
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza Mafunzo Unganishi(Bridging Course) na Kozi Awali(Pre-Entry Course)wakiwa makini kusikiliza hotuba ya Mgeni rasmi,mafunzo yatawawezesha kujiunga na mafunzo ya Stashahada(Diploma) ya Uandisi katika Chuo cha Ufundi Arusha.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika akimpongeza mmoja wa wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo,Aneth Chotto wakati akijiandaa kupokea Cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho,Abraham Nyanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Abraham Nyanda akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo.
Uongozi wa Chuo katika picha ya pamoja na wahitimu wa kike wanaotarajiwa kujiunga katika ngazi ya Stashahada ya Uandisi.