Friday, July 18, 2014

TIMU YA TANZANIA KATIKA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA YATUA JIJINI GLASGOW, SCOTLAND


TIMU YA TANZANIA KATIKA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA YATUA JIJINI GLASGOW, SCOTLAND
 Timu ya Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland jana usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).
 Jumla ya wanamichezo 42 waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa  na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. Pamoja na mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao.
 Bw. Msanjila akimlaki  Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. Katikati ni Kiongozi wa Msafara Bw. Muharami Mchume 

 Bw. Msanjila akimkabidhi bendera ya Tanzania Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. 

Baadhi ya Watanzania na marafiki zao waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao. Michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumatano (23 Julai 2014) na Malkia Elizabeth wa Pili itajumuisha nchi na Himaya 70. Michezo hiyo itafungwa tarehe 3 Agosti 2014.