Thursday, July 10, 2014

RAIS KIKWETE ALIPOKABIDHIWA KITAMBULISHO NAMBA 1 CHA USHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA (DITF) KUTOKA MAXMALIPO .


RAIS KIKWETE ALIPOKABIDHIWA KITAMBULISHO NAMBA 1 CHA USHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA (DITF) KUTOKA MAXMALIPO .
Rais  Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akabidhiwa kitambulisho Maalumu cha kielektoniki kwaajili ya Kuingia katika Maonesho ya 38 ya biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kutika Kwa bwana Ahmed Lussasi Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo

Rais. Jakaya Mrisho alipata Nafasi ya kuzungumza na Maafisa wa Maxmalipo Juu ya Mfumo wa Kieletroniki wa Ticket (e-Ticketing System) uliofungwa na Maxmalipo Katika viwanja Vya Sabasaba. Pia Mheshimiwa Rais alijionea Jinsi Mfumo huu unavyodhibiti na kuboresha Ukusanyaji wa Mapato katika msimu huu wa Maonesho ya sabsaba. Mfumo huu wa kisasa pia Unauwezo wa kusimamia mapato katika nyanja mbalimbali kwa kutumia Barcode technology pia na Facial detection.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lusasi akifafanua Jambo kwa Mh. Dr. Jakaya Mrisho wakati alipo Tembelea Banda la Maxmalipo ndani ya Viwanja vya sabasaba.
 Mh.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (Rais) Akitizama kwa Umakini na kupata maelekezo Juu ya mfumo wa kielektoniki wa Ticket unavyotumika sabasaba na unavyowezakutumika sehemu Mbalimbali.